UBALOZI WA URUSI NCHINI TANZANIA WAKUTANA NA VIONGOZI WA WIZARA YA UTALII NA MAMBO YA KALE JIJINI DAR ES SALAAM

Wizara ya Utalii Na Mambo ya Kale imekutana na Balozi wa Urusi nchini Tanzania *Hon. YURI F. POPOV *na kufanya nae Mazungumzo kuhusiana na Utalii pamoja na Uwekezaji ndani ya Sekta hiyo.

Kikao hicho kimefanyika leo huko jijini Dar es salaam wakati Mhe. Lela alipomtembelea balozi huyo na kufanya nae mazungumzo mafupi.

Aidha Mhe. Lela amesema Zanzibar na Urusi wamekua na Mahusiano Mazuri hasa katika kipindi hiki cha Mlipuko wa janga la korona (corona ) ambapo wageni wengi wamekua na hofu ya kufanya Utalii kutoka nchi moja kwenda nyengine. Mhe. Lela amefafanua kwamba Urusi imekua ni miongoni mwa nchi zilizoweka Imani na Zanzibar na kuonekana wageni wengi wanaotoka Urusi wanatembelea Visiwa hivi jambo ambalo limeleta Matumaini na kuufanya Utalii wa Zanzibar kuzidi kutangazika ndani na nje ya nchi.

Aidha Mheshimiwa Lela amelezea kuwa, Pamoja na Changamoto Mbali mbali zilizomo ndani ya Utalii ila bado Wageni wanaendelea kuvutiwa na Zanzibar hasa kwa Vivutio vinavopatikana ndani ya Visiwa hivi vya Unguja na Pemba.

Mheshimiwa Lela Amesema kwamba ipo haja kwa balozi huyo kutembelea na kuangalia Vivutio vinavopatikana ndani ya Visiwa hivyo pia kuzijua Fursa za Uwekezaji zinazotolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa chini ya Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Nae balozi wa Urusi nchini Tanzania Hon. YUFI F. POPOV Amefurahishwa sana na juhudi zinazofanywa na Serikali hii ya awamu ya nane,Pia Amempongeza sana Raisi wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa Uongozi wake anaoendelea kuiongoza Zanzibar .

Aidha ameahidi kua ataendelea kuunga mkono juhudi za serikali kwa kutoa Mashirikiano Mazuri ndani ya Sekta hiyo ya Utalii jambo ambalo litafungua mianya ya kuleta Uchumi endelevu nchini Tanzania.

Ikumbukwe kuwa Mnamo tarehe 21/10/2020 Na kuendelea Zanzibar imekua ikipokea jumla ya wageni zaidi ya 2000 kutoka Urusi walio wasili na ndege aina tofauti ikiwemo Charter Skyup Airlene, wageni 232. Nordwind Airlines, wageni 440. Azur Air, wageni 525. Boeing 777 Royal flight, Wageni 485. UT air na nyenginezo kupitia katika Uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume.

Mawasiliano yetu

Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale
Mnazi Mmoja, Zanzibar.
S.L.P 2277, Zanzibar.
Barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
Tovuti: www.utaliismz.go.tz